Friday, February 3, 2012

NINACHOJIVUNIA BAADA YA MAFUNZO


Ni siku tano sasa zimekamilika tangu tunze kupewa mafunzo ni kwa namna gani mimi kama mwandishi naweza tumia mtandao katika kazi zangu za kila siku ili niwe mfanisi na kufanya akzi za uhakika.


Mafunzo haya yameandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari vilivyo kusini mwa Afrika MISA-TAN kwa kushirikian na Wizara ya mambo ya nje ya Finland ikiwa na lengo la kuwawezesha watumishi walio katika taasisi za kutoa habari kuwa na uwezo wa kutumia mtandao na kutoa habari  kwa njia ya mtandao ili kufikia hadhira kubwa.

Kikubwa nilichojifunza katika mafunzo haya ni kwa namna mtandao umeweza kubadili jamii na mfumo
mzima wa mawasiliano duniani kwa kiasi kikubwa na takiwmu zinaonyesha kuwa watumiaji wa mtandao ulimwenguni wanaongezeka kila siku jambo ambalo linakuwa ni changamoto katika tasnia ya vyombo vinavyochapisha habari.

Lakini  kikubwa zaidi nilichojifunza kulingana na mada zilizojadiliwa na mwalimu na darasa kwa ujumla, ni kwa namna gani nitakuwa mwandishi wa kisasa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya utoaji wa habari kwa njia ya mtandao.

Vyanzo hivyo vinaweza kuwa vya kitaifa na kimataifa vitaniwezesha kufanya tafiti zangu kwa ufasaha  ikiwa ni pamoja na kupata takwimu na maelezo sahihi ya kile nitakachokuwa nakitafuta kwa wakati huo.

Katika mafunzo haya nimebaini changamoto kubwa inayokabili nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na kusababisha kuwa nyuma katika masuala ya maendeleo ya sayansi na teknolojia  na  matumizi ya matandao ni mfumo duni wa elimu uliopo nchini,uanzishawaji na teknolojia ambazo watu hawana ujuzi katika kuvitumia na miundo mibovu isyoruhusu kwa urahisi matumizi ya mtandao.

Ukiacha hayo kingine nilichojifunza ni kwa namna gani naweza kutumia mtandao kuchukua habari na maelezo pasipo kunukuuu kazi za watu  kinyume na sheria au idhini kutoka kwa mmiliki wa chanzo hicho cha habari(Plagralism and Copyrights).

Ninachojivunia zaidi ni kupitia mafunzo haya nimeweza kucreate blog yangu ambayo naamini nitaendelea kuifanyia kazi kama njia mojawapo ya kuwasiliana na jamii ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuleta mabadiliko masuala ya jamii,uchumi na siasa

No comments:

Post a Comment